Matamshi ya hivi punde yanaashiria kuongezeka kwa hatari katika mojawapo ya maeneo tete duniani. Huku mvutano ukipamba moto baada ya shambulio baya katika Kashmir inayotawaliwa na India, pande zote mbili zinaonekana kukaribia makabiliano ya kijeshi ambayo yanaweza kuzusha hali ya wasiwasi katika eneo lote na kwingineko.
Mvutano kati ya India na Pakistan unazidi kuongezeka siku moja baada ya serikali mjini Islamabad kusema ina taarifa za uhakika za kiintelijensia kwamba India inapanga kuishambulia ndani ya siku chache zijazo.
Waziri wa Habari wa Pakistan, Attaullah Tarar alinukuliwa jana akisema kwamba nchi yake ina taarifa za kuaminika za kiintelijensia kwamba India inakusudia kufanya shambulizi la kijeshi dhidi ya Pakistan ndani ya masaa 24 hadi 36 yajayo, hilo likiwa tishio la hivi karibuni zaidi la vita kati ya majirani hao wawili wenye silaha za nyuklia.
Mvutano wa India na Pakistan unaambatana na harakati za kijeshi zinazoendelea kuongezeka kwenye mpaka wa nchi kavu wa nchi hizo mbili jirani.
Mzozo wa sasa kati ya New Delhi na Islamabad umeibuka baada ya watu waliokuwa na silaha kulifyatulia risasi kundi la watalii katika eneo la kitalii la Pahalgam, lililoko takriban kilomita 90 kutoka Srinagar, mji mkuu wa majira ya joto wa Kashmir inayodhibitiwa na India, na kuua watu wasiopungua 27, Jumanne ilioyopita.
342/
Your Comment